Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi kati ya Azam na Yanga itakayochezwa Jumapili (Septemba 14) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000...>>>>
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho cha sh. 5,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani na bluu vitakavyochukua jumla ya watazamaji 36,000 katika uwanja huo wenye viti 57,558.
Viingilio vingine katika mechi hiyo ambayo itatumia tiketi za elektroniki ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa viti vya VIP C na B wakati viti vya VIP A kiingilio ni sh. 30,000.
0 comments:
Post a Comment