Polisi nchini Ujerumani wamefanikiwa kumkamata promota mwenye asili ya nchi ya Nigeria ambaye ndiye aliyesababisha fujo katika onyesho la msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ zilizotokea Agosti 30 mwaka huu kwenye ukumbi mmoja mjini Stuttgart nchini Ujerumani...>>>
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka nchini Ujerumani kilisema kwamba Jeshi la Polisi nchini humo kilisema hadi kieleweke kwani watamchukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa mapromota kama huyo.
Jumamosi iliyopita Awin Williams Akpomie (pichani) alisababisha fujo na kuvunjwa kwa viti, vyombo vya muziki na vitu mbalimbali baada ya mashabiki kushikwa na hasira kwa kukosa burudani ya shoo ya Diamond ambapo alicheleweshwa na promota huyo aliyewatangazia shoo kuanza kufanyika saa nne usiku na badala yake kutaka shoo ifanyike saa kumi alfajiri.
Na Blogu ya Wananchi.
0 comments:
Post a Comment