Top 10 ya rekodi za ada kubwa za usajili wa wachezaji kwa muda wote.

Kila mwishoni mwa msimu wa Ligi mbalimbali duniani vilabu husika huwa na utamaduni wa kuanza kufuatilia wachezaji sahii watakao ongeza nguvu katika vilabu vyao na namna ambavyo watawapata. Siku hizi kila klabu inapomuhitaji mchezaji kutoka klabu moja kwenda nyingine uhamisho wake uhitaji ada kubwa kutokana na kiwango cha mchezaji husika.
0

Klabu mbalimbali duniani imekuwa kawaida sana kukuta wakinunua mchezaji kwa gharama ya juu, Real Madrid wao huwa hawajali gharama ya mchezaji bali huwa wanaangalia ni kweli wanamuhitaji na anauwezo wa kusaidia timu yao basi hawaoni ugumu kuingia mfukoni na kutoa mamilioni ya pound ili tu kuhakikisha wanampata mchezaji wamtakaye na kuboresha kikosi chao.
Nimeona nikusogezee mtu wangu wa nguvu Top 10 ya wachezaji walio katika rekodi ya gharama ya usajili kwa muda wote.
10. Radamel Falcao pamoja na klabu nyingi kuwa zinamuwania wakati huo akiwa katika klabu ya Atletico Madrid ya Hispania, pound milioni 51 zilitosha kwa klabu ya Monacokuipiku klabu ya Chelsea na zingine zilizokuwa zinamuwania mshambuliaji huyo waColombia na kufanikisha kumpleleka UfaransaFalcao kwa sasa anaichezea klabu yaChelsea ya Uingereza kwa mkopo.
tran5afp_2650536k
9. Ni Edinson Cavani mshambuliaji wa kimataifa kutokea Uruguay ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa uhamisho wake wa Pound milioni 55 kutoka katika Klabu ya Napoli ya Italia kwenda PSG upo katika hi rekodi.
tran4epa_2650534k
Edinson Cavani
8. Ricardo Kaka uhamisho wake wa pound milioni 56 kutoka katika klabu ya AC Milankwenda katika klabu ya Real Madrid ya Hispania uliingia katika rekodi ya klabu hiyo na hata kwa wachezaji wengine waliowahi kusajiliwa kwa dau kubwa. Kaka kwa sasa anaichezea klabu ya Orlando City.
tran3reu_2650533k (1)
Ricardo Kaka
7. Zlatan Ibrahimovic mwaka 2009 alikuwa ni headlines katika kila chombo cha habari kinachojiuhusisha na utoaji wa habari za michezo, baada ya kusajiliwa kwa dau la pound milioni 59 kutoka katika klabu ya Inter Milan na kujiunga na FC Barcelona ya Hispania,Zlatan kwa sasa anaichezea klabu ya PSG.
tran2ap_2650532k
Zlatan Ibrahimovic
6. Angel Di Maria uhamisho wake wa pound milioni 59.7 kutoka Real Madrid kwenda katika klabu ya Man United ya Uingereza haukuwa ni rekodi katika klabu ya Man Unitedpekee ila umeingia katika list ya wachezaji waliosajiliwa kwa fedha nyingi. Di Maria kwa sasa yupo katika klabu ya PSG aliyojiunga nayo msimu huu.
dimariahead_3017006k
Angel Di Maria
5. James Rodriguez mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, michuano ya Kombe la dunia 2014 iliyofanyika Brazil ili ongeza thamani yake kwani ni moja kati ya wachezaji waliyocheza kwa kiwango cha juu hivyo Real Madrid hawakuona ugumu kutoa pound milioni 63 na kuilipa Monaco kwa ajili ya staa huyo.
James_Rodriguez_2982918k
James Rodriguez
4.Vilabu vingi viliwania saini ya Neymar bila mafanikio ila klabu ya FC Barcelonainayosifika kwa kuibua vipaji ilikubali kulipa pound milioni 71.5 na kumsajili nyota huyo kutoka katika klabu ya Santos ya Brazil.
neymarget_3017000k
Neymar
3.Mwaka 2014 ndio mwaka ambao klabu ya FC Barcelona ilifanikiwa kumnasa nyota waLiverpool wakati huo Luis Suarez kwa dau la pound milioni 75 na kumfanya staa huyo kutua Nou Camp.
Uruguay v Jordan - FIFA World Cup Qualifiers...MONTEVIDEO, URUGUAY - NOVEMBER 20: Luis Suarez of Uruguay runs with the ball during leg 2 of the FIFA World Cup Qualifier match between Uruguay and Jordan at Centenario Stadium Stadium on November 20, 2013 in Montevideo, Uruguay. (Photo by Friedemann Vogel/Getty Images)
Luis Suarez
2. Uhamisho wa Cristiano Ronaldo kutoka Man United kwenda Real Madrid uliingia katika headlines kwani ulikuwa wa dau kubwa na ukilinganisha na jina lake Ronaldo.hivyo pound milioni 80 zilitosha Man United kushawishika kumuuza staa huyo.
tran1reu_2650530k
Cristiano Ronaldo
  1. Gareth Bale alikuwa katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza ni mmoja kati ya wachezaji wenye kasi zaidi hivyo umahiri wake uwanjani uliwafanyaReal Madrid ya Hispania kutoa pound milioni 86 na kuilipa Spurs ili wapate baraka za kumnasa nyota huyo.
    bale_2650561k
    Gareth Bale
CHANZO: telegraph.co.uk
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks