Waziri mkuu wa zamani Frederick Tluway Sumaye ametangaza rasmi kuhamia CHADEMA (Ukawa) leo asubuhi.
Sumaye, 65, aliwahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania kuanzia Novemba 28, 1995 hadi Desemba, 30, 2005 wakati wa uongozi wa rais wa amamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa.
Msomi huyo wa Harvard amesema kuwa anajiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ili kuimarisha upinzani.
Frederick Sumaye anakuwa kiongozi wa pili wa juu kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhamia Chadema (Ukawa) baada ya Edward Lowassa ambaye alikihama chama hiko mapema mwezi Agosti na kuteuliwa kugombea urais kupitia chama hiko katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 25, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment