Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM lililokutana tarehe 15.08.2015 katika ukumbi wa Julius Nyerere International convention centre limemvua uanachama wa ukamanda mkuu mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru.
Mbali na hilo, umoja huo uliazimia mambo mengine yafutayo:-
1. Kikao pia kiliunda timu ya kampeni ambayo itafanya kazi pamoja na kamati ya utekelezaji kuhakisha ushindi wa CCM kwa nafasi zote.
2. Kikao kimemshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba nzuri ya ufunguzi wa Baraza na kikao kimeahidi kutekeleza maagizo na maelekezo ya hotuba hiyo kwa matendo.
0 comments:
Post a Comment