Maamuzi ya Waziri Mwakyembe baada ya ajali iliyotokea mkoani Mara


Jana September 5 2014 kwenye eneo la Sabasaba hapa Musoma ilitokea ajali mbaya sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na kulihusisha gari jingine dogo ambapo majeruhi ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39 Wanawake kwa Wanaume kwa mujibu wa taarifa mpya za vifo zilizotoka muda mfupi uliopita.>>>>..

Kwa kuguswa na tukio hili waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe ilibidi aahirishe ratiba zake nyingine na kulazimika kuja Musoma kuwatembelea majeruhi leo asubuhi kwenye hospitali ya mkoa pamoja na kwenda kwenye eneo la ajali kutazama.
Baada ya hapo Waziri Mwakyembe akaongea na Chanzo cha habari na kueleza yafuatayo >>
Inabidi niwape pole Watanzania wote ambao wamepoteza ndugu jamaa na marafiki, taarifa za ajali nimezipata nikiwa Dodoma kwenye bunge maalum ikawa sasa nitafikaje haraka Musoma kwa hiyo ikabidi nitafute ndege leo asubuhi kuja hapa’
Kuhusu Wasanii wa bongofleva na Clouds Media Group kufanya maamuzi ya kuahirisha tamasha ambalo lilikua lifanyike jana hapa Musoma, Waziri Mwakyembe amesema >> ‘hii imenifurahisha sana… inaonyesha Utanzania tulionao Watanzania, ni vizuri wamefanya hivyo na ninawapongeza sana Clouds Radio kwa kuguswa na maswala ya jamii’

‘Ajali sasa hivi Tanzania zimechukua nafasi ya yale magonjwa tunayoyaogopa hasa kwa kuchukua maisha ya watu na kujeruhi na kuiingizia serikali gharama kubwa ya matibabu, hatuwezi kuliangalia hili swala hivihivi mimi kama Waziri wa uchukuzi nimewaambia wenzangu kuanzia sasa Watanzania wataona mabadiliko makubwa’ - Dr. Mwakyembe
  1. Tunaanza na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku anamuona mwenzake na kusema mimi lazima anipishe’ – Dr. Mwakyembe
  2. Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha zao lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya kupeleka abiria yaendeshwe na watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa kila dereva kwamba amejiunga na hii mifuko ya akiba ya Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi’
  3. Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu binadamu…. bila comprehensivehaendeshi mtu gari kuchukua abiria.

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks