Mifupa ya Dinosaria (Dinosaurs) yapatikana Tz Rukwa

baadhi ya mifupa ya  mnyama huyo iliyopatikana huko mkoani Rukwa
Aina mpya ya Dinosaria (Dinosaurs)  imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania.
Mabaki hayo ya Dinosaria yaliyopewa jina la – ‘Rukwatitan Bisepultus’ – yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa, kusini magharibi mwa nchi hiyo...>>>>

baadhi ya mifupa ya mnyama huyo iliyopatikana huko mkoani Rukwa
Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa akiishi kwa kula majani, aliishi karibu miaka  milioni 100 moja iliyopita, na alikuwa na uzito sawa na tembo kadhaa na alikuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa mita mbili.
Mnyama huyo ni aina ya Titanosaurus ambao ni wakubwa, na wanaokula nyasi.Gorscak etal_Fig 3_Silhouette
Mabaki ya wanyama aina hiyo mpaka sasa yamepatikana katika maeneo ya Amerika ya Kusini, bara ambalo lilijitenga kutoka Afrika katika kipindi cha Cretaceous,
(kipindi ambacho miamba ya chokaa iliumbika) takriban miaka milioni mia moja na arobaini iliyopita.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks