Mhitimu wa shahada alishika bango linalotangaza ujuzi wake kwa wapita njia kwenye kituo cha Waterloo, amepata kazi anayoitaka baada ya kushindikana kuipata kwa njia iliyozoeleka (barua)..>>>
Alfred Ajani, 22, alihofia kutofanikiwa baada ya kuomba kazi zaidi ya 300 bila mafanikio baada ya kuhitimu masomo yake mwezi Mei.
Siku moja aliamka mapema na kwenda kwenye eneo linalopita wafanyakazi wengi wa jiji la London, akishika bango linalosema: “Mhitimu wa masoko- uliza CV tafadhali.”
Mbinu yake ilipokelewa vizuri na wakurugenzi wanaopita ila kiongozi mmoja alimuona na hatimaye kumpatia kazi.
Alfred, anayetokea London kusini, alianza kazi ya masoko kwenye kampuni ya usajili ya Asoria Group jana na sasa anafanya kazi kutoka kwenye eneo ambalo alisimama wakati akitafuta kazi.
Alisema: “Kiongozi alinipita pale na kuniona ile asubuhi, niliamua kutafuta mawasiliano yake kwenye mtandao wa Linked In.”
Kwa wahitimu vyuo wanaotafuta kazi jijini Dar es Salaam, ukiona mambo yamegonga mwamba, barua hazijibiwi si dhambi kwenda eneo la Posta na kumuiga Alfred Ajani.
0 comments:
Post a Comment