Diamond Platnumz na Yemi Alade kutoka Nigeria ambaye amefanya vizuri na ngoma yake ya Johnyy, wamesaini mkataba na chama cha haki miliki cha nchini Kenya. MCSK.
Wasanii hao walikuwa nchini humo katika shughuli za kurekodi kipindi cha Coke Studio Africa msimu wa pili..>>>>>>
“Tulimkabidhi Diamond cheki ya fedha nyingi za mirahaba baada ya kumuonyesha michakato yetu, alikuwa tayari kusaini nasi” alisema CEO wa MCSK, Maurice Okoth
kwa sasa diamond ndio msanii maarufu wa nje na msanii wa nje aliyepata fedha nyingi za mirahaba. Yemi alikuwepo pembeni wakati tunamuonyesha Diamond hatua za kusaini na yeye akafurahishwa sana na ofa yetu na hapo ndipo tulimsainisha pia.
Maurice alidai kuwa tuzo za MCSK zitafanyika October 20 kwenye hoteli ya Safari jijini Nairobiambapo diamond, Jose Chameleone, Eric Wainaina,M.O.G Bahati, P-Unit, Size 8 na Bahati ni miongoni mwa wasanii watakaohudhuria.
0 comments:
Post a Comment