Somalia wamewekewa mashine ya kwanza ya kutolea pesa (ATM) katika mji mkuu, Mogadishu.
Baadhi ya watu wanachanganywa na namna mashine hiyo inavyofanya kazi kwa sababu hawakuwahi kutumia hapo awali, ameripoti Mohamed Moalimu wa BBC kutoka katika mji huo....>>>
Mashine hiyo, imewekwa na Benki ya Salaam Somali katika hoteli ya soko la juu, inaruhusu wateja kutoa dola za Kimarekani.
Somalia ina sekta ndogo ya kibenki, huku watu wengi wakitegemea malipo ya pesa kutoka kwa watu kutoka nje.
Maendeleo yake yamekuwa yakiathiriwa na vita vya zaidi ya miongo miwili vinavyohusisha koo na makundi ya wanamgambo wa kidini.
0 comments:
Post a Comment