Mwakilishi wa Kenya nje ya Big Brother

Baada tu ya wiki mbili katika nyumba ya Big Brother Mwakilishi
mmoja wa Kenya Sabina ametimuliwa.
Sabina ana mtoto wa miezi minane na ndio mkenya wa kwanza
kutimuliwa kutoka katika nyumba hiyo.
Inadaiwa kuwa watazamaji na mashabiki wa makala hiyo waliamua
kumuondoa Sabina baada ya siku 14 pekee ili aende kumuhudumia
mwanawe.
Sabina alionekana kumkosa sana mwanawe na wakati mwingi
alionekana akifunga vitu kwenye mgongo wake ungedhani
anambeba mtoto.
Sabina alionekana kuwa kipenzi cha wengi
Aliweka pamoja blanketi na nguo na kuvifunga kwenye mgo wake
akiwa na kofia ya mwanawe huku akitembea katika nyumba hiyo
kabla ya kujiunga na wenzake waliokuwa wakijivinjari nje.
Baadhi wanasema kufunga vitu mgon
goni ndio chanzo za mashabiki
kuanza kuomuonea huruma Sabina wakisema bora aende nyumbani
kwa mwanawe mwenye miezi minane.
Na hapo ndipo walipompigia kura Jumapili na kumtimua kutoka
katika Big Brother house.
Sabina alitimuliwa kutoka katika nyumba hiyo pamoja na Lilian
kutoka Nigeria na Esther wa Uganda.
Hatua ya kumondoa Sabina katika Big Brother house inamwacha
mwakili mmoj tu wa Kenya Melvin Alusa ambaye ni kakake Ben
aime Baraza wa kikundi cha wanamuziki cha Sauti Sol.

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks