Kuanzia leo longo longo ya kwamba sikuupata ujumbe wako wa
WhatsApp itakuwa historia, au kudai kuwa ujumbe haujafika
utakuwa unaongopa mchana kweupe.
Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu
zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa, tick mbili
za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa, na tick
mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe
uliotumwa
Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea Pressing
and holding an individual message shows the Message Info
option
Ukibofya utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
Maoni kuhusu mabadiliko hayo yamepokelewa tofauti katika
mitandao ya kijamii, wapo ambao hawajafurahishwa
Whatsapp haijatoa sababu za kufanya mabadiliko hayo ambayo
yamewakera baadhi ya watumiaji.
Kuanzia jana huduma hiyo inayomilikiwa na Facebook- itakuwa
ikionyesha tick mbili za rangi ya blue upande wa chini kulia
katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa umesomwa.
Na ukibofya ujumbe wenyewe utaona muda kamili ambao
mlengwa alifungua na kuusoma ujumbe husika.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment