Leo katika historia Jumamosi, Februari 28, 2015


Jumamosi, Februari 28, 2015
Leo ni Jumamosi tarehe 9 Mfunguo Nane Jamad al-Awwal 1436 Hijria inayosadifiana na tarehe 28 Februari mwaka 2015 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 24 iliyopita, George Bush "baba" alitangaza usitishaji vita vya Ghuba ya Uajemi vilivyodumu kwa muda wa siku 40. Mgogoro huo ulianza mwezi Agosti 1990 baada ya majeshi ya Iraq kushambulia ghafla sehemu ya ardhi ya Kuwait na kuikalia kwa mabavu. Ndege za kijeshi za Marekani, Uingereza na Ufaransa zilianza kuyashambulia majeshi ya Iraq baada ya utawala wa Saddam Hussein kukataa amri ya kuyaondoa majeshi yake nchini Kuwait.***
Miaka 93 iliyopita katika siku kama ya leo , nchi kongwe ya Misri ilipata uhuru. Misri ilikombolewa na Waislamu miaka 20 baada ya kudhihiri dini tukufu ya Kiislamu. Mwaka 969 nchi hiyo ilidhibitiwa na kutawaliwa na silsila ya Fatimiyya hadi mwaka 1172 ambapo utawala huo ulipinduliwa na Waayyubi. Baada ya hapo Misri ilidhibitiwa na tawala tofauti. Waingereza walianza kuwa na ushawishi huko Misri katika miongo ya mwishoni mwa karne ya 19. Hata hivyo wananchi wa Misri walikabiliana na ukoloni wa Uingereza na mwanzoni mwa Vita vya Kwanza vya Dunia hapo mwaka 1914 Uingereza iliitangaza Misri kuwa chini ya himaya yake. Wananchi wa Misri walidumisha mapambano ya uhuru baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia na kuilazimisha Uingereza kuutambua rasmi uhuru wa nchi hiyo hapo mwaka 1922. ***
Katika siku kama ya leo miaka 90 iliyopita, Ayatullahil Udhma Sayyid Abu Turab Khonsari aliaga dunia. Khonsari alikuwa mmoja wa wasomi na maulama wakubwa na mashuhuri wa Iran. Alizaliwa huko Khonsar moja ya miji ya katikati mwa Iran na baada ya kumaliza masomo yake ya awali ya kidini alielekea katika Chuo Kikuu cha Kidini mjini Isfahan na baadaye huko Najaf Iraq. Ayatullah Khonsari alikuwa ametabahari pia katika uga wa uandishi wa vitabu na vitabu vya Misbahus Swalihiin na Qasdus Sabiil ni baadhi tu vitabu vyake mashuhuri.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks