Wimbi la kumshawishi Lowassa kugombea lapamba moto


Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli Edward Lowassa
Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli Edward Lowassa
Wimbi la watu kumuunga mkono na kumshawishi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kugombea nafasi ya urais wakati utakapofika, limezidi kupamba moto na safari hii, ujumbe mzito kutoka Pemba unajiandaa kufanya hivyo.
Taarifa za maandalizi kwa wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Pemba kwenda Monduli kumshawishi Lowassa kugombea urais, zimekuja siku chache baada ya baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kanda ya Ziwa, kufanya hivyo wiki iliyopita.
Wananchi hao katika kutimiza dhamira yao, walimtuma Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho taifa, Dk. Raphael Chegeni, kwenda kumshawishi Lowassa ili awanie nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Monduli jana,  Mjumbe wa Halmashauri ya chama hicho taifa, (NEC) kutoka Wilaya ya Chake Chake Pemba, Daud Ismali, alisema amekwenda Monduli kumshawishi Lowassa kugombea nafasi ya urais muda utakapofika.
Ismail ambaye ni mdogo wa Makamu wa Rais, marehemu, Dk. Omar Ally Juma, alisema kwenda kwake Monduli kufanya maandalizi ya ujumbe mzito utakao toka Pemba kwenda kumshawishi agombee urais.
“Watakuja kumwomba mheshimiwa Lowassa kugombea urais, uamuzi wa kugombea au kutogombea ni wake.
Akieleza kwanini waje kumshawishi Lowassa badala ya mtu mwingine, alisema ni kutokana na utendaji na uadilifu wake.
Pia alisema, “jina la mheshimiwa ni kubwa na siyo Pemba tu hata ukienda Marekani ukiuliza ni jina gani linazungumzwa kuhusu urais utaambiwa ni Lowassa.”
“Ukienda mtaani kukusanya data za aina yo yote ile, jina linalotajwa kuwa linafaa kuwania nafasi hiyo ni la Lowassa,” alisema.
Chanzo: NIPASHE
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks