Leo katika historia Jumanne, Februari 24, 2015

Jumanne, Februari 24, 2015

Jumanne, Februari 24, 2015
Leo ni Jumanne tarehe 5 Jamadil Awwal 1436 Hijria sawa na tarehe 24 Februari 2015.
Siku kama ya leo miaka 1431 iliyopita alizaliwa Bibi Zainab (s.a) binti mtukufu wa Imam Ali bin Abi Twalib na Bibi Fatimatu Zahraa (as). Bibi Zainab alikuwa mashuhuri miongoni mwa watu kutokana na maarifa na elimu kubwa aliyokuwa nayo. Katika tukio la Karbala, Bibi Zainab (s.a) alisimama kidete na kukabiliana na dhulma za watawala dhalimu na ujahili watu wa zama hizo ili kutimiza malengo matukufu ya kaka yake, Imam Hussein (a.s). Bibi Zainab alipelekwa Sham pamoja na mateka wengine wa Nyumba Tukufu ya Mtume (saw) baada ya mapambano ya Imam Hussein (a.s) huko Karbala. Hotuba za Bibi Zainab mbele ya majlisi ya Ibn Ziyad mtawala wa Kufa na katika ikulu ya Yazid bin Muawiya huko Sham zilikuwa na taathira kubwa katika kufichua dhulma na ukandamizaji wa Bani Umayya na kuonesha jinsi Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume walivyodhulumiwa.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa nchini Iran siku ya kuzaliwa Bibi Zainab (a.s) husherehekewa kama 'Siku ya Wauguzi'.
Miaka 167 iliyopita katika siku kama ya leo, utawala wa muda au duru ya pili ya utawala wa Jamhuri nchini Ufaransa ilianza kufuatia mapambano yaliyoanzishwa na wananchi wa Ufaransa na kujiuzulu Louis Philippe, mfalme dhalimu wa nchi hiyo. Mfumo huo wa utawala unatajwa pia katika historia ya Ufaransa kwa jina la utawala wa waandishi wa habari wa magazeti kutokana na kuwa, waandishi wa habari kumi na moja wa magazeti wakiongozwa na Alfonso de la Martin aliyekuwa malenga na mwandishi, ndio waliokuwa wakiongoza utawala huo.
Na siku kama ya leo miaka 66 iliyopita, ulitiwa saini mkataba wa kuacha mapigano kati ya wawakilishi wa Misri na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kisiwa cha Rhodes katika bahari ya Aegean. Baada ya kuundwa dola haramu la Israel katika ardhi ya Palestina hapo mwaka 1948, Misri pamoja na nchi nyingine za Kiarabu, iliingia katika vita dhidi ya utawala huo bandia. Hata hivyo jeshi la Israel lilishambulia vikosi vya Waarabu ambavyo havikuwa na zana za kisasa za kivita na kuingia katika ardhi za Misri na Lebanon baada ya kuvishinda vikosi hivyo. Vita hivyo vilimalizika Januari mwaka 1949 ambapo katika tarehe kama ya leo pande mbili zilitia saini mkataba wa kuacha vita chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa. Nchi nyingine za Kiarabu pia zikaukubali mkataba huo. Kwa mujibu wa mkataba huo eneo la Ukanda wa Gaza liliwekwa chini ya mamlaka ya Misri.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks