Marekani iliwasilisha mapendekezo kwa Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo Sudan Kusini ambayo imeshindwa kusitisha vita ya miezi 14.
Hatua hizo zilitumwa kwenye Baraza la Usalama siku moja baada ya Ethiopia kufungua ukurasa wa makubaliano kati ya pande zinazopigana zilizotolewa kama fursa ya mwisho kufikia makubaliano.
Chini ya mapendekezo hayo, Baraza la Usalama linaweza kuweka vikwazo vya kusafiri duniani na kupiga tanji mali za watu wanaohatarisha utulivu wa Sudan Kusini.
Pendekezo hilo linaweza kuweka vikwazo vya silaha nchini Sudan Kusini, hatua inayoungwa mkono na nchi za Ulaya pamoja na kwamba adhabu hiyo inaweza kuviadhibu vikosi vya Rais Salva Kiir zaidi ya wapiganaji wa muasi Riek Machar.
“Viongozi wa siasa wameshindwa kuweka ajenda zao za siasa na uchumi pembeni ili kutafuta suluhisho la kisiasa ambalo litaweza kuleta utulivu,” alisema afisa wa Marekani.
0 comments:
Post a Comment