Rais Robert Mugabe: Nilikuwa sitaki kuwa rais


Rais wa Zimbabwe na Mwenyeikiti wa Umoja wa Afrika Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe na Mwenyeikiti wa Umoja wa Afrika Robert Mugab
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kiongozi wan chi mzee barani Afrika, amedai kuwa hakuwahi kutaka kuwa rais pamoja kuwa madarakani kwa miaka 35.
Rais Mugabe, ambaye alifikisha miaka 91 Jumamosi iliyopita, alifanya sherehe za kuzaliwa kwenye ofisi yake siku ya Jumatatu na kueleza kwamba alikataa kukubali nafasi za juu katika harakati za ukombozi Zimbabwe kabla ya uhuru.
Alikuwa kiongozi wa kwanza wa Zimbabwe huru mwaka 1980 akiwa kama Waziri Mkuu kabla kupewa urais mwaka 1987.
“Sikujiunga na mapambano kwa sababu nilitaka siku moja kuwa Waziri Mkuu, hapana, ila nilijiunga na mapambano kutimiza wajibu wangu kama ulivyoelezwa kwenye chama, kwanza kama katibu wa uenezi na kama tulivyohama kutoka NDP, ZAPU, bado nilikuwa katibu uenezi,” alisema.
“Nilikuwa katibu mkuu wa chama na nilibakia hivyo hata mpaka pale watu walipoamini kuwa kiongozi wa chama amekuwa msaliti,  Ndabaningi Sithole, huku baadhi ya watu wakiwa gerezani, Tekere Nyagumbo, tulibakia kadhaa na mwenyewe na hawa watatu walitaka mimi nitangazwe kuwa kiongozi wa chama ila nilikataa.”
“Nilikataa hata nilipotoka gerezani tulikubaliana kuwa wale wote waliokamatwa waachiwa na waliachiwa kabla ya Mkutano wa Geneva na bado nilikuwa katibu mkuu,” aliongeza Mugabe.
“Hoja yangu ilikuwa, rais anaweza kuchaguliwa na watu, lakini mwaka 1977 tulikuwa na mkutano huo Chimoio, nilikubali kwa sharti moja kwamba tutapambana uhalali kutoka kwa watu tutakaporudi nyumbani. Ila nilikuwa natimiza wajibu wangu.”
Mugabe pia ameadhinishwa kuwa mgombe urais kwenye uchaguzi wa 2018 ambapo atakuwa na miaka 94.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks