Matumizi ya Bangi yahalalishwa


miki
Matumizi ya Bangi ya halalishwa jimbo la Alaska Marekani
Kwetu TZ kila siku unakutana na taarifa za watu kukamatwa na bangi, dawa za kulevya, hizi ni kesi ambazo tunazisikia na kuzisoma kila siku kwenye vyombo vya habari, Marekani iko tofauti kidogo.
Alaska linakuwa jimbo la tatu kuhalalisha matumizi ya Bangi ndani ya Marekani, unaruhusiwa kuvuta, kulima na hata ukikutwa na bangi sio ishu kabisa yani kwao.
Kuna baadhi ya viongozi ambao wameanza kuwa na wasiwasi kwamba kama wakati ule wakati bado haijahalalishwa ishu za mauaji na watu kukamatwa kwa makosa ya kufanya vurugu zilikuwa
kwa kiwango cha juu sana, sasa hivi imeshakuwa halali ni nini kitaendelea hasa wakiangalia kwamba kwenye hizo kesi, matumizi ya bangi na pombe yametajwa kuchangia sana.
Bangi ni ruhusa kwa sasa kwenye Jimbo hilo ila marufuku ni moja tu, huruhusiwi kuvuta hadharani, basi.
Majimbo yaliyotangulia kuruhusu hii ni Washington na Colorado, Jamaica nayo imo kwenye list ya nchi zilizo kwenye hatua za mwisho kupitisha sheria inayoruhusu bangi.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks