Bara la Afrika laongoza kwa kutoa chakula bora duniani


Baadhi ya matunda yanayopatikana nchini Chad
Baadhi ya matunda yanayopatikana nchini Chad
Kwa mujibu wa utafiti wa kimataifa uliofanywa kuhusu lishe bora bara la Afrika limeongoza katika kutoa chakula bora licha ya kuwepo uhaba wa chakula.
Kwa mujibu wa jarida la afya la The Lancet Global Health la Marekani nchi ya Chadi ndiyo imeongoza kwa kutoa chakula chenye lishe bora hiyo imetokana na nchi hiyo kutumia asilimia kubwa ya matunda,mboga za majani na nafaka mbalimbali.
Nchi nyingine ni kama Sierra Leone, Mali, Gambia, Uganda, Ghana, Ivory Coast, Senegal na Somalia.
Kwa mujibu wa habari iliotolewa katika tovuti ya The Lancet Global Health ni kwamba chakula katika mataifa ya magharibi kina athiri afya kutokana upishi wake wa haraka.
Dr Imamura muasisi wa utafiti huo alisema kuwa watu wazima hula vizuri kuliko vijana, na wanawake kuliko wanaume.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi hao wamesema kuboresha mlo ni muhimu sana ili kuweza kupiga vita magonjwa yasiokuwa ya kuambukiza ambayo yamekadiriwa kusababisha vifo kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2020.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks