Aliyemuua mwamuzi ahukumiwa kifungo cha miaka 8


Mke wa mwamuzi aliyeuawa kwa kupigwa ngumi akimuonesha kadi nyekundu mchezaji aliyemuua mme wake
Mke wa mwamuzi aliyeuawa kwa kupigwa ngumi akimuonesha kadi nyekundu mchezaji aliyemuua mme wake
Mchezaji wa soka Bassel Saad amehukumiwa kwenda jela kwa miaka 8 baada ya kumpiga ngumi na kumuua refa katika mechi ya Ligi ya Soka ya Michigan United.
John Bieniewicz alikuwa anataka kumuonesha Bassel Saad kadi ya pili ya njano kabla ya  kumtoa nje kwa kadi nyekundu.
Mchezaji huyo mwenye miaka 37 kabla hajatolewa nje ya uwanja alimuwahi mwamuzi huyo na kumdunda ngumi moja tu ya uso na kumuacha refa akiwa amezirai.
Mwamuzi huyo alikuwa na miaka 44, alifariki siku mbili baada ya mechi hiyo iliyochezwa mwezi Juni huko Detroit.
Saad amekubali makosa ya kuua bila kukusudia na juzi ijumaa alihukumiwa kwenda jela miaka minane.
Wakati Saad akiwa anataka kuondolewa mahakamani, mjane wa Bwana Bieniewicz, Kristen alinyanyua kadi nyekundu na kusema: “Ningependa kumpa kadi nyekundu Bwana Saad ambayo alistahili kupewa.” Saada pia ameamuriwa kulipa dola elfu 9 za gharama za mazishi.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks