Beki mahiri wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amejiondoa
kwenye kikosi hicho kitakachopambana na Platinum ya Zimbabwe katika
mchezo wa kombe la shirikisho Afrika ambao utafanyika wikiendi hii
kwenye uwanja wa taifa.
Cannavaro amesema amejiondoa kwenye kikosi hicho baada ya kupata
majeraha juu ya jicho la kushoto na kusababisha kushonwa nyuzi saba.
Nahodha huyo ameongeza kuwa, matibabu ya jicho lake aliyapata siku ya
Jumatatu asubuhi kwenye Hospitali ya Kilwa Road, Kurasini jijini Dar es
salaam mara baada ya mechi hiyo kumalizika.
Aliongeza kuwa, hataweza kucheza kutokana na maumivu makali
anayoyasikia kwenye jeraha hilo, hivyo ameona ni vyema akapumzika hadi
jeraha hilo litakapopona kabisa kwa hofu ya kujitonesha.
“Ninatamani kucheza mechi na Platnum, lakini kutokana na jeraha hili kiukweli sitaweza kucheza maana nina hofu kijitonesha”.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment