Leo katika historia Jumatano, Machi 11, 2015

Jumatano, Machi 11, 2015
Leo ni Jumatano tarehe 20 Jamadi Awwal 1436 Hijria sawa na Machi 11, 2015.
Siku kama ya leo miaka 9 iliyopita, Slobodan Milosevic dikteta wa Yugoslavia ya zamani aliaga dunia akiwa korokoroni mjini Hague huko Uholanzi. Milosevic alitiwa mbaroni mwaka 2001 miezi tisa baada ya kuanguka utawala wake na kukabidhiwa kwa mahakama ya watenda jinai wa Yugoslavia ya zamani huko Hague. Slobodan Milosevic alijiunga na chama cha Kikomonisti cha Yugoslavia ya zamani akiwa kijana na kuwa Rais wa Jamhuri ya Serbia mwaka 1989. Dikteta huyo wa Yugoslavia ya zamani alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kushiriki katika mauaji ya umati dhidi ya maelfu ya Waislamu wa Bosnia.
Miaka 11 iliyopita katika siku inayosadifiana na ya leo, miripuko ya mabomu matano ilitokea kwa wakati mmoja katika vituo kadhaa vya treni za chini ya ardhi au metro huko Madrid mji mkuu wa Uhispania na kuua karibu watu 200 na kujeruhi wengine 1000. Miripuko hiyo ilitambuliwa kuwa operesheni kubwa zaidi ya kigaidi kuwahi kutokea nchini Uhispania na Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Japokuwa serikali ya mrengo wa kulia ya Uhispania ililituhumu kundi linalotaka kujitenga eneo la Basque la ETA kuwa ndilo lililohusika na mashambulizi hayo ya kigaidi lakini kundi la al Qaida lilitoa taarifa likisema kuwa ndilo lililotekeleza hujuma hiyo. 
Na miaka 30 iliyopita katika siku inayosadifiana na hii ya leo, mgogoro mkubwa katika ngazi za uongozi wa Urusi ya zamani ulifikia kikomo kufuatia kutangazwa kifo cha Konstantin Chernenko na badala yake Mikhail Gorbachev ambaye wakati huo alikuwa mwanachama kijana zaidi katika ofisi ya kisiasa ya chama cha Kikomunisti akatangazwa kuchukua nafasi ya Chernenko. Hatua ya kuchaguliwa Gorbachev kuongoza chama hicho cha Kikomunisti ilikwenda sambamba na kujiri mabadiliko makubwa, ambayo hatimaye yalipelekea kusambaratika Umoja wa Kisovieti.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks