Ufisadi mwingine wa mabilioni wagundulika Wizara ya Ujenzi
Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya (CAG) katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.
Kutokana na ufisadi huo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amependekeza hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika wa Wizara ya Ujenzi na wakala wa barabara ili kuleta imani na uwazi kwa jamii na wahisani kuhusu bajeti ya nchi.
0 comments:
Post a Comment