Leo Katika Historia Ijumaa, 13 Machi, 2015

 http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/1f080291b576d2767fdfd1ab65bef037_XL.jpg
Leo ni Ijumaa tarehe 22 Jamadil Awwal 1436 Hijria sawa na Machi 13, 2015.
Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita inayosadifiana na tarehe 22 Esfand 1358 Hijria Shamsia, Imam Ruhullah Khomeini MA alitoa amri ya kuundwa taasisi ambayo itakuwa ikishughulikia hali za familia za mashahidi waliouawa wakitetea Mapinduzi ya Kiislamu nchini. Taasisi hiyo hadi sasa bado inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kiutamaduni, kijamii na kiuchumi kwa familia za mashahidi wa harakati za mapinduzi na hali kadhalika familia za mashahidi wa vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na Iraq dhidi ya Iran.
Siku kama ya leo miaka 282 iliyopita, yaani 13 Machi, 1733 alizaliwa Joseph Priestley, mkemia na mwanafizikia wa Uingereza. Msomi huyo aliishi katika kipindi kilichokuwa maarufu kama zama za dhahabu za kemia na elimu hiyo ilikuwa imepiga hatua. Katika uchunguzi na utafiti wake, Priestley alivumbua uvutaji pumzi katika mimea na gesi za ok
sijeni na haidrojeni. Joseph Priestley alifariki dunia mwaka 1804.
Na miaka 852 iliyopita katika siku kama hii ya leo, alifariki dunia Muhammad bin Jazmi Hamedani mwenye laqabu ya Zainuddin, mpokezi wa hadithi na hafidhi wa Qur’ani Tukufu. Katika zama zake hakuwa na mfano katika elimu ya hadithi, kuhifadhi hadithi na aya za Qur’ani Tukufu. Jazmi kwa kipindi cha miaka 35 ya maisha yake aliandika vitabu vingi ikiwa ni pamoja na Al Iitibar fi al Nasikh Walmansukh” na “Silsilatu Dhahab”.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks