Leo ni Jumamosi tarehe 23 Mfunguo Nane Jamad al-Awwal 1436 Hijria ambayo inasadifiana na tarehe 14 Machi mwaka 2015 Miladia.
Siku
 kama ya leo miaka 37 iliyopita yaani tatrehe 14 Machi 1978, jeshi la 
utawala wa Kizayuni wa Israel lilianza kuivamia na kuikalia kwa mabavu 
ardhi ya Lebanon kwa kisingizio cha kukabiliana na operesheni 
iliyofanywa na wanamapambano wa Kipalestina pambizoni mwa Tel Aviv. 
Katika mashambulio hayo jeshi la Israel liliua raia wengi wasio na hatia
 wa Lebanon na Palestina na kuikalia kwa mabavu sehemu ya ardhi ya 
Lebanon. Hata hivyo utawala huo ghasibu uliondoka kwa fedheha katika 
maeneo ya kusini mwa Lebanon mwaka 2000 baada ya kupata kipigo kikali 
kutoka kwa wanamapambano shupavu wa Harakati ya mapambano ya Kiislamu ya
 Hizbullah na kuondoka kwenye eneo hilo.***
Katika siku kama ya leo 
miaka 136 iliyopita, alizaliwa nchini Ujerumani Albert Einstein, msomi 
mashuhuri wa fizikia na hisabati. Mnamo mwaka 1921 msomi huyo mahiri 
alipewa tuzo ya Nobel katika taaluma ya fizikia, baada ya kufanya juhudi
 kubwa za kiutafiti. Utafiti na nadharia za Einstein katika uwanja wa 
nyuklia zilikuwa na taathira kubwa duniani. Hata hivyo Einstein 
alisikitika sana baada ya kugundua kwamba, uchunguzi na utafiti wake 
umetumiwa na baadhi ya nchi kwa ajili ya kutengeneza silaha hatari za 
nyuklia. Albert Einstein alifariki dunia mwaka 1955. ***
Na miaka 129
 iliyopita katika siku kama ya leo kulingana na kalenda ya Hijria, 
aliaga dunia Sayyid Muhammad Ibrahim mashuhuri kwa lakabu ya Sayyidul 
Ulamaa, alimu na fakihi wa Kiislamu wa nchini India. Alikuwa mmoja wa 
maulama watajika na mahiri mwanzoni mwa karne ya 14 Hijria. Baada ya 
kufariki dunia baba yake, Muhammad Ibrahim alichukua jukumu la baba yake
 la kueneza mafundisho ya dini katika baadhi ya miji ya India. 
Mwanazuoni huyo alifanya hima kubwa ya kueneza misingi na itikadi za 
Kiislamu katika ardhi ya India
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
                            (
                            Atom
                            )
                          
 
 

0 comments:
Post a Comment