Pele: Baada ya Messi na Ronaldo ni Neymar


Pele: 'baada ya Messi na Ronaldo ni Neymar'
Pele amesema baada ya Ronaldo na Messi, anafuata Neymar
Katika mahojiano aliyoyafanya na waandishi wa gazeti la L’Uomo Vogue Gwiji wa soka duniani Pele, amemtaja Cristiano Ronaldo kama mwanasoka bora duniani kwasasa baada ya utawala wa miaka mingi wa Mwaargentina Lionel Messi 27, na huku akidai kuwa ufalme wa Neymar katika soka ndio utakaofatia baada ya ule wa Cristiano na Messi.
Gwiji huyo anaimani kuwa siyo muda mrefu kutoka sasa nyota wa Brazil pamoja na klabu ya Barcelona Neymar Jr. 23, ndiye atakaye kuwa mtawala mpya wa soka na ndiye tegemeo la timu yake ya taifa pamoja na klabu yake.
Pia mshindi huyo wa Kombe la Dunia mara tatu aliulizwa juu ya ubora uliopo kati ya wachezaji wa kizazi chake na hawa wakisasa alisema, “nadhani suala teknolojia mpya za kisasa haliwezi kumfanya mwanasoka awe bora ila ni kipaji pamoja na mapenzi aliyonayo mchezaji katika soka,”
Ninaamini hata kama ningezaliwa katika kizazi hiki bado ningekuwa mwanasoka bora hivyo sidhani kama kuna sababu ya wanasoka wa kizazi changu kushindwa kung’ara katika soka la kisasa.”
Pamoja na mafanikio makubwa aliyoyapata gwiji huyo katika soka lakini bado anajiona kama mwanasoka asiyetimia katika maisha yake ya soka kutokana na kuikosa michuano ya Olimpiki.
Pamoja na kutokupata nafasi ya kucheza mpira katika uwanja maarufu duniani wa Wembley uliopo katika Jiji la London Uingereza
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks