Kesi ya Mbunge wa Bahi kuunguruma Aprili 29


Mbunge Omary Badweli akiwa mahakamani
Mbunge Omary Badweli akiwa mahakamani
Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam imesema kuwa itatoa hukumu ya Kesi ya rushwa inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Bahi mkoani Dodoma Omary Badweli Aprili 29, mwaka huu.
Badwel anakabiliwa na shitaka la rushwa ambalo anadaiwa kutenda kati ya Mei 30 na Juni 2, 2012, katika maeneo tofauti mkoani Dar es Salaam ambapo alishawishi apewe rushwa ya Shilingi Milioni 1 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Sipora Liana.
Kesi hiyo imedumu kwa takribu miaka mitatu sasa inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi Hellen Riwa ambapo hukumu hiyo itatolewa baada ya mahakama hiyo kusikiliza na kupitia ushahidi wote uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka na utetezi pamoja na vielelezo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, inadaiwa Badwel aliomba rushwa hiyo ili kushawishi wajumbe wengine wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kupitisha hesabu za halmashauri hiyo ambapo pia Juni 2, 2012 katika hoteli Peacock jijini Dar es Salaam alipokea rushwa ya Shilingi Milioni 1 kutoka kwa Sipora ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga mkoani Pwani.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks