Kuhusu Chelsea kupata dili nono la jezi


Wawakilishi wa kampuni ya Yokohama ambao ndio wadhamini wapya wa klabu ya Chelsea wakiwa katika Picha ya pamoja akiwemo kocha mkuu Jose Mourinho
Wawakilishi wa kampuni ya Yokohama Rubber ambao ndio wadhamini wapya wa klabu ya Chelsea wakiwa katika Picha ya pamoja akiwemo kocha mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho.
Klabu ya Chelsea imetangaza kusaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya Yokohama Rubber wakiwa ndiyo wadhamini wapya wa matangazo ya jezi.
Mkataba huo wenye thamani ya pauni mil 40 ( Tsh Bil 108) kwa mwaka unaifanya Chelsea kuwa klabu ya pili katika matangazo ya jezi katika vilabu vya Uingereza
huku Manchester United wakishika namba moja kwa kuingiza pauni mil 53 kwa mwaka kutokana na mkataba wao wa miaka saba na kampuni ya magari ya Chevrolet .
Chelsea imekuwa ikidhaminiwa na kampuni ya Samsung tangu mwaka 2006 ambao walikuwa wanaiingizia klabu hiyo pauni mil 18 kwa mwaka.
Kampuni hiyo kutoka Tokyo nchini Japan ambayo inashughulika na utengenezaji wa matairi,vifaa vya majini na ujenzi wa viwanda
pia inadhamini vilabu mbambali vinavyoshiriki ligi kuu ya kikapu nchini Marekani Nba kama vile Bolton,Celtic na San Antonio Spurs.
‘Karibuni sana wadhamini wetu wapya Yokohama, ninaamini mahusiano yetu yatakuwa na faida sana na tutafika mbali zaidi ‘alisema mwenyekiti wa klabu ya Chelsea Bruce Buck.
Hivyo Chelsea ambao wapo kileleni katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza wataanza kuvaa jezi zilizoandika Yokohama rubber kuanzia msimu wa 2015/2016.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks