Kuhusu Utoro kushamiri bungeni


Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akizungumza bungeni
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akizungumza bungeni
Utoro kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa umekithiri baada ya ofisi ya bunge hilo kusema kuwa wana taarifa  za wabunge 15 tu walioomba ruhusa kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
Bunge hilo, linalotakiwa kuwa na wabunge 357, na kuna miswada ambayo ilishindwa kupitishwa kutokana na upitishwaji wake kuhitaji theluthi mbili za wabunge wa kila upande wa muungano kati ya bara na visiwani.
Wakati wa mjadala wa muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa ambao uliwasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), Jenister Mhagama kulikuwa na idadi ya wabunge 81 tu bungeni, jambo ambalo linasikitisha kutokana na umuhimu wa hicho chombo.
Hali ilikuja kuwa mbaya zaidi juzi wakati wa kujadili Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi, kulikuwa na wabunge 29 tu ukumbini.
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge,  John Joel alimwambia mwandishi wetu kuwa wana taarifa ya wabunge 15 ambao wanaruhusa kutoka kwa spika ya kutoshiriki kwenye vikao vinavyoendelea.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks