Leo katika historia Jumamosi, Machi 21, 2015

Jumamosi, Machi 21, 2015

Leo ni Jumamosi tarehe 30 Mfunguo Nane Jamad al-Awwal 1436 Hijria sawa na tarehe 21 Machi 2015 Miladia.
Leo ni tarehe Mosi Farvardin mwaka mpya wa 1394 Hijria Shamsia ambayo inasadifiana na siku ya kwanza ya mwaka wa Kiirani maarufu kwa jina la Sikukuu ya Nowruz. Nowruz ni moja kati ya sherehe za kale zaidi duniani na ilianza kusherehekewa zaidi ya miaka 3000 iliyopita. Mwaka 2010 Umoja wa Mataifa ulitangaza rasmi Machi 21 (yaani tarehe Mosi Farvardin) kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Nowruz. Umoja wa Mataifa umeitambua Siku ya Nowruz kama siku kuu ya kale ambayo huadhimishwa wakati wa kuwadia msimu wa machipuo na kuhuishwa tena mazingira. ***
Katika siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, nchi ya Kiafrika Namibia ilipata uhuru kutoka kwa Afrika Kusini na siku kama hiii huadhimishwa kama siku ya taifa. Historia ya ukoloni huko Namibia inarejea katika karne ya 19. Wakoloni wa Kijerumani, Kiingereza na Kireno mwishoni mwa karne ya 19 walianzisha mashindano ya kupora na kudhibiti maliasili na utajiri wa Namibia. Hata hivyo mkoloni Kijerumani ndiye aliyefanikiwa kuidhibiti na kuikoloni nchi hiyo. ***
Miaka 47 iliyopita katika siku kama ya leo, kulitokea mapigano makubwa kati ya Harakati ya PLO ya Palestina na majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Karama ulioko Jordan. Kwa uchache wanajeshi 1,230 wa Kizayuni waliangamizwa na makumi ya vifaru kutekelezwa au kuchukuliwa ngawira na wanamapambano wa Kipalestina kwenye mapigano hayo. Harakati ya PLO ilianza kupoteza hadhi yake ya kimapambano baada ya kulegeza misimamo yake ya kimapinduzi mwaka 1991 na kukubali kuketi kwenye meza ya mazungumzo ya amani na utawala ghasibu wa Israel; mazungumzo ambayo hayajawa na matunda yoyote kwa wananchi wa Palestina. ***
Na miaka 49 iliyopita katika siku kama ya leo, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO liliitangaza siku ya mauaji ya umati dhidi ya wazalendo weusi nchini Afrika Kusini yaliyotokea mwaka 1960 kuwa "Siku ya Kimataifa ya Kufuta Ubaguzi wa Rangi". Waafrika weusi wapatao 69 waliuawa na wengine 180 kujeruhiwa katika siku kama ya leo, baada ya askari wa makaburu kuwafyatulia risasi watu hao waliokuwa wakiandamana kwa amani huko Sharpeville nchini Afrika Kusini. ***

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks