Leo katika historia Ijumaa, 20 Machi, 2015





Leo ni Ijumaa tarehe 29 Jamadi Awwal 1436 Hijria sawa na Machi 20, 2015.
Siku kama ya leo miaka 12 iliyopita sawa na tarehe 20 Machi 2003, Marekani na Uingereza kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na silaha za mauaji ya halaiki kwa pamoja ziliishambulia Iraq na kuuangusha utawala wa Saddam Hussein. Mashambulio hayo yalipingwa na walimwengu ambao walizituhumu nchi hizo za Magharibi kwa kuchukua hatua hiyo kinyume cha sheria kwa lengo la kudhamini maslahi yao haramu katika eneo la Mashariki ya Kati. Hatua hiyo iliitumbukiza nchi ya Kiislamu ya Iraq katika mikono ya vikosi wavamizi kwa miaka kadhaa.
Siku kama ya leo miaka 64 iliyopita, sawa na tarehe 29 Esfand 1329 Hijria Shamsia, baada ya vuta nikuvute na mapambano ya wananchi wa Iran dhidi ya mkoloni Mwingereza na utawala kibaraka wa mfalme hapa nchini, hatimaye wabunge wa Bunge la Taifa na lile la Seneti walipitisha muswada wa kutaifisha sekta ya mafuta nchini. Kupitishwa muswada huo ilikuwa hatua muhimu katika mapambano ya wananchi wa Iran dhidi ya mkoloni Mwingereza. Kufuatia kupasishwa sheria hiyo, Muswadiq aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Iran kwa kuungwa mkono wa wananchi na viongozi wa kidini hasa Ayatullah Kashani.
Na tarehe 20 Machi miaka 288 iliyopita, alifariki dunia Isaac Newton mwanafizikia, mwanahisabati na mwanafikra wa Kiingereza akiwa na umri wa miaka 84. Alizaliwa mwaka 1643 na kusoma katika Chuo Kikuu cha Cambridge. Akiwa na umri wa miaka 24, Isaac Newton alifanikiwa kugundua kanuni muhimu ya makanika. Newton alibainisha pia sheria tatu za mwendo yaani (Three laws of motion) katika kitabu chake alichokipa jina la Mathematical Principles of Natural Philosophy.

Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks