Leo katika Historia Jumanne, Machi 17, 2015



Jumanne, Machi 17, 2015
Leo ni Jumanne tarehe 26 Jamadi Awwal 1436 Hijria sawa na 17 Machi 2015.
Miaka 1379 iliyopita inayosadiafina na siku kama ya leo, ardhi ya Baitul Muqaddas huko Palestina ilikombolewa na Waislamu. Vita vya kwanza kati ya Waislamu na Warumi vilijiri huko kaskazini mwa Bahari Nyekundu baada ya kudhihiri Uislamu. Jeshi la Waislamu lilitoa pigo kwa Warumi na eneo la kusini mwa Palestina likakombolewa katika zama za utawala wa Umar bin Khattab. Baada ya kushindwa huko, mfalme wa Roma alituma jeshi kubwa katika ardhi za Palestina. Warumi walishindwa vibaya na jeshi la Kiislamu katika vita vilivyojiri huko Palestina na mwishoni mwa mapigano hayo, kamanda wa jeshi la Roma aliuawa na Damascus ikadhibitiwa na Waislamu.
Siku kama ya leo miaka 81 iliyopita, alifariki dunia Ayatullah Allamah Mirza Muhammad Hussein Naini, marjaa na faqihi mkubwa na mmoja wa wahakiki wa elimu ya usulu fiq’h. Allamah Naini alizaliwa mwaka 1276 Hijiria Qamaria mkoani Nain, ambao ni moja ya mikoa ya katikati mwa Iran katika familia ya kidini. Allamah Naini alisoma na kuhitimu masomo yake ya awali nyumbani kwao na kuendelea na masomo ya juu huko mjini Najaf, Iraq. Akiwa mjini hapo, alipata kusoma kwa wasomi wakubwa wa zama hizo kama vile Allamah Mirza Shirazi na kufikia daraja ya juu ya elimu za hesabu, falsafa ya sayansi, falsafa, irfan na fiq’hi. Miongoni mwa athari za Allamah Naini ni pamoja na vitabu vya “Wasiilatun-Najjat” na “Tanbiihul-Ummah wa Tanziihul-Millah” kitabu ambacho kilitoa mchango mkubwa katika kuathiri mapambano dhidi ya viongozi dhalimu wa zama hizo.
Miaka 20 iliyopita katika siku kama leo, alifariki dunia Sayyid Ahmad Khomeini mwana wa kiume wa mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini M.A. Ahmad Khomeini alizaliwa mwaka 1324 Hijria Shamsiya na akapata malezi na elimu kutoka kwa baba yake. Hujjatul Islam Sayyid Ahmad Khomeini alikuwa na nafasi muhimu katika kuanzisha mawasiliano na kuwa kiunganishi kati ya Imam Khomeini M.A na wanamapinduzi hapa nchini. Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia Sayyid Ahmad Khomeini alijisabilia kulinda mapinduzi hayo na katika kipindi cha miaka 6 ya baada ya kufariki dunia baba yake alifanya jitihada kubwa kutete misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu na Kiongozi Muadhamu wa mapinduzi hayo Ayatullah Ali Khamenei.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks