LEO KATIKA HISTORIA: Machi 22


Muhammad Ali


1967 – Muhammad Ali alimtandika Folley KO
Bondia Cassius Marcellus Clay Jr. ‘Muhammad Ali’ alimzibua Zora Folley na kutwaa ubingwa wa dunia. Muhammad Ali alizaliwa Januari 17, 1942 hadi sasa ana umri wa miaka 73. Alijiunga na dini ya Kiislamu 1975 . Zora alifariki Julai 9, 1972 akiwa na umri wa miaka 41 akishinda mapambano 6 ya kijeshi ndani ya mwaka mmoja. Pia alishiriki vita ya Korea (1950-1953).

1972 –Kareem Abdul- Jabbar, alitunukiwa MVP
Ferdinand Lewis Alcindor ‘Kareem’ alitajwa kuwa mchezaji bora wa kikapu (MVP) nchini Marekani. Alizaliwa Aprili 16, 1947 New York nchini Marekani.  Sasa ana miaka 67,  aliwahi kuzitumikia klabu za Milwaukee Bucks na Los Angeles Lakers. Alitwaa mara 6 MVP pia amewekwa katika kumbukumbu za zama zote za Chama cha Kikapu nchini Marekani (NBA).

2013 – Ray Williams alifariki
Thomas Ray Williams alizaliwa Oktoba 14, 1954 Mount Vernon nchini Marekani. Alikuwa mchezaji wa kikapu (NBA) kuanzia mwaka 1977 – 1987. Alifariki kwa matatizo ya kansa ya utumbo jijini New York. Alihudhuria masomo yake katika chuo cha San Jacinto Junior kisha akaichezea timu ya Chuo Kikuu cha Minnesota mwaka 1975 – 1977 .
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks