LEO KATIKA HISTORIA: Machi 24

Undertaker

 1889: Albert Hill alizaliwa
Alikuwa mkali wa kufukuza upepo kutoka Uingereza ambaye alitwaa medali mbili za dhahabu katika mita 800 na 1500 kwenye michuano ya Olimpiki mwaka 1920. Alizaliwa Tooting, jijini London. Aliwahi kulitumikia jeshi na alishiriki Vita vya Kwanza vya Dunia. Alifariki dunia Januari 8, 1969. Mwaka 2010 alipewa heshima katika ‘England Athletics Hall of Fame’.

1913: Uholanzi ilipata ushindi wa kwanza dhidi ya England
Timu ya soka ya Uholanzi iliikung’uta  kwa mara ya kwanza England mabao 2-1 mjini De Haag, kusini mwa Uholanzi. Mabao ya ‘Oranje’ yalifungwa na Huug de Groot. Mpaka sasa wamekutana mara 31. Kwa mara ya kwanza walikutana Aprili 1, 1907 Uholanzi ilizabwa mabao 8-1.

1965: Undertaker alizaliwa
Jina halisi la mwanamieleka huyu ni Mark William Calaway, sasa amesaini mkataba mwingine na WWE ambao alianza nao tangu mwaka 1990. Anajulikana kwa majina mengi anapokuwa ulingoni  miongoni mwa hayo ni ‘The Phenom’, ‘The Punisher’, ‘The Master of Pain.’
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks