Klabu ya Real Madrid imewapiga marufuku mashabiki watatu kuingia uwanjani baada ya siku ya jumatatu kulishambulia gari la mshambuliaji wa klabu hiyo Gareth Bale.
Inasemekana kuwa mashabiki hao walikuwa wamekaa nje ya uwanja wa mazoezi wakiwasubiria wachezaji wa klabu hiyo ambao siku ya jumapili walitoweka ghafla baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa mahasimu wao Barcelona.
Wanaume hao walionekana kwenye video wakiwatukana na kushambulia magari ya wachezaji wa timu hiyo.
Baada ya mkutano wa kinidhamu kumalizika klabu hiyo ilitoa taarifa ya kuwafungia mashabiki hao kujihusisha na mambo ya klabu hiyo.

0 comments:
Post a Comment