Leo katika historiaJumapili, 24 Jamadil Awwal 1436 Hijria


Jumapili, 24 Jamadil Awwal 1436 Hijria
Leo ni Jumapili tarehe 24 Jamadil Awwal 1436 Hijria sawa na tarehe 15 Machi 2015 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 161 iliyopita alizaliwa tabibu maarufu wa Kijerumani kwa jina la Emil Adolf von Behring. Baada ya kumaliza masomo yake Behring aliendeleza utafiti wa Louis Pastor, mwanakemia wa Kifaransa wa zama hizo katika uwanja wa kutambua na kuzuia maradhi yanayoambukiza na kubahatika kufikia mafanikio makubwa katika uwanja huo. Kufuatia hali hiyo Emil Adolf von Behring akatunukiwa tuzo ya Nobel katika taaluma ya fizikia hapo mwaka 1901. Emil alifariki dunia mwaka 1917 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 110 iliyopita, alitiwa mbaroni na hatimaye kuuawa na vibaraka wa mtawala Muhammad Ali Shah Qajar wa Iran, Mirza Nasrullah Malakul-Mutakallimin, mwandishi, khatibu na mpigania uhuru mkubwa. Mirza Nasrullah alizaliwa mjini Isfahan Iran mwaka 1277 Hijiria. Mwaka 1299 Hijiria alifanya safari nchini India. Kutokana na athari ya matatizo yaliyokuwa yakiwakabili watu wa jamii ya India yaliyokuwa yakisababishwa na utawala wa kikoloni wa Waingereza kwa nchi hiyo, jambo hilo lilimpelekea msomi huyo kusambaza kitabu chake cha kwanza alichokipa jina la 'Minal-Khalq ilal-Haqqi'. Kitabu hicho kilipewa nafasi kubwa na maulama na raia wengi wa India, huku kikiibua hasira kali ya naibu mtawala wa Kiingereza aliyekuwa akiongoza taifa hilo. Ni kutokana na hali hiyo ndipo akakamatwa na kubaidishwa katika moja ya miji ya Iran.
Siku kama ya leo miaka 26 iliyopita ardhi ya Taba iliyoko kaskazini mashariki mwa Misri ilikombolewa baada ya kukaliwa kwa mabavu kwa miaka kadhaa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Utawala wa Kizayuni ulilikalia kwa mabavu jangwa la Sinai katika vita vya mwaka 1967, ambalo upande wa mashariki mwake linapatikana eneo la Taba. Utawala wa Tel Aviv ulikubali kuirejeshea Misri jangwa la Sinai baada ya kusaini mkataba wa Camp David mwaka 1987. Israel iliendelea kulikalia kijeshi eneo muhimu la Taba huko kaskazini mwa Ghuba ya Aqaba, licha ya utawala huo wa Kizayuni kuondoka katika baadhi ya sehemu za jangwa hilo.
Na siku kama ya leo miaka 30 iliyopita vibaraka wa kigeni sanjari na kutega bomu katika mkusanyiko mkubwa wa wananchi Waislamu wa Iran katika sala ya Ijumaa ya mjini Tehran, walipelekea idadi kubwa ya waumini kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Tukio hilo la kigaidi na kijinai lilienda sambamba na kujiri vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo ndege za utawala huo wa Kibaathi nchini Iraq, zilikuwa zikipaa kwenye anga ya jiji la Tehran. Nukta ya kuzingatia ni hii kwamba, shambulio hilo halikuweza kusimamisha shughuli hiyo ya kisiasa na kiibada ambapo Ayatullahil-Udhmaa Sayyid Ali Khamenei, aliyekuwa akihutubu, aliendelea na kutoa hotuba hiyo na kuongoza sala katika hali ya utulivu wa kinafsi.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks