Leo katika historia Jumatatu, Machi 16, 2015


Jumatatu, Machi 16, 2015

Leo ni Jumatatu tarehe 25 Jamadil Awwal mwaka 1436 Hijria sawa na tarehe 16 Machi 2015 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 156 iliyopita kulingana na kalenda ya Miladia, Alexander Stepanovich Popov, mvumbuzi na mwanafizikia wa Russia alizaliwa. Baada ya kuhitimu masomo yake katika taaluma ya fizikia, alianza kujishughulisha na ufundishaji katika vyuo vikuu vya nchi hiyo. Mbali na shughuli hiyo, Popov aliendelea mbele na utafiti wake katika nyanja mbalimbali za kielimu ambapo baadaye alifanikiwa kuvumbua chombo cha kunasia sauti na kukipa jina la kinasia sauti. Aliaga dunia mwaka 1906.***
Siku kama ya leo miaka 66 iliyopita, alifariki dunia Ayatullah Mirza Mohammad Feiz Qumi; msomi, ustadh na Marja mkubwa wa Kiislamu katika mji wa kidini wa Qum hapa nchini Iran. Ayatullah Feiz Qumi alizaliwa na kukulia katika mji huo wa Qum na baada ya masomo na utafiti wake wa kina katika mji wa Najaf nchini Iraq alifikia daraja ya Ijtihad. Baadaye alirudi katika mji wa Qum ambako alikuwa akitoa mafunzo ya dini tukufu ya Kiislamu kabla ya kuaga dunia mjini hapo katika siku kama ya leo.***  
Siku kama ya leo miaka 76 iliyopita, alifariki dunia Bi Selma Lagerlof mwandishi wa Sweden. Lagerlof alizaliwa mwaka 1858 na baada ya kumaliza masomo yake akaanza kujishughulisha na ukufunzi na uandishi wa hadithi na hekaya. Lagerlof alikuwa mwanamke wa kwanza kutunukiwa tuzo ya Nobel katika fani ya fasihi mwaka 1909.
Na siku kama ya leo miaka 38 iliyopita, kikosi cha Red Brigade kilimteka nyara Aldo Moro Waziri Mkuu wa zamani wa Italia. Moro alikuwa mfuasi wa chama cha Kidemokrasia cha Kikristo cha Italia na kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwa duru tano. Wanachama 65 wa Brigedi Nyekundu walimuuwa mwanasiasa huyo takriban miezi 2 baada ya kumteka nyara. Brigedi Nyekundu lilikuwa kundi la mrengo wa kushoto lenye misimamo ya kufurutu ada huko nchini Italia lililokuwa likiitaka nchi hiyo kuachana na taasisi za Magharibi khususan Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi NATO.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks