Ndege moja ya shirika la ndege la Lufthansa la Ujerumani kwa jina la German Wings imeanguka nchini Ufaransa.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320 iliyoanguka nchini Ufaransa inaarifiwa kumilikiwa na shirika la ndege la Lufthansa nchini Ujerumani.
Shirika la Umma la Wanaanga la Ufaransa limetangaza kuanguka kwa ndege hiyo katika eneo la Barcelonette lililoko kusini mwa Ufaransa wakati ilipokuwa ikielekea mjini Dusseldorf Ujerumani kutoka Barcelona Uhispania.
Ndege hiyo iliripotiwa kupoteza mawasiliano jana jioni abiria 142 pamoja na wahudumu 6 wanasadikiwa kupoteza maisha
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametoa maelezo kuwa, ‘’Sidhani kama kuna mtu yeyote aliyepona.’’
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve ameelekea katika eneo la tukio.
Bado hakuna taarifa yoyote yaliyotolewa kuhusiana na abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.

0 comments:
Post a Comment