Wadau wa habari wataka serikali isiwatenge miswada ya Haki ya Kupata Taarifa na Huduma za Vyombo vya Habari

Bunge la Tanzania
Inadaiwa serikali inakusudia kupenyeza miswada hiyo kwa njia ambayo ni ya dharura badala ya kawaida. Lengo la mpango huo halijaeleweka.
Kumekuwa na pilika nyingi miongoni mwa wadau wa sekta ya habari Tanzania kutaka serikali itambue ukiukwaji wa demokrasia ambao unadaiwa kutaka kutokea kuhusu uwasilishwaji wa miswaada miwili yenye utata katika bunge linaloendelea mjini Dodoma.
Wakati miswada miwili ya habari ya mwaka 2015, ule wa Haki ya Kupata Taarifa na mwingine wa Huduma za Vyombo vya Habari ikitarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo chini ya hati ya dharura, wadau wa habari wamewasilisha ombi maalum kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, wakimuomba atumie hekima zake kuishauri serikali kuiwasilisha katika mfumo wa kawaida.
Kwa mujibu wa maombi hayo, wadau hao ambao wameweka kambi mjini Dodoma tangu Jumamosi iliyopita, wamemuomba Spika kutumia madaraka yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi kuishauri serikali kuwasilisha miswada hiyo katika utaratibu wa kawaida ili kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kabla ya kupitishwa kuwa sheria.
Barua pia imeandikwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye ni Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ikimuomba naye aone umuhimu wa wananchi kushiriki kutoa maoni katika miswada hiyo kabla ya kupitishwa na Bunge kwenye mkutano wa 19 unaoendelea mjini Dodoma.
Naye Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freema Mbowe, ameandikiwa barua na wadau hao wakimuomba atumie nafasi yake kama msemaji mkuu wa kambi hiyo bungeni kuishauri serikali iwasilishe miswada hiyo chini ya mfumo wa kawaida na siyo chini ya hati ya dharura kwani unawanyima wananchi fursa ya kutoa maoni yao kwenye miswada hiyo kabla ya kupitishwa na Bunge.
Tangu serikali iseme kuwa inakusudia kuwasilisha miswada hiyo chini ya hati ya dharura, wadau wa habari wamekuwa wakiomba ibadili msimamo kwani kufanya hivyo kutawanyima wananchi fursa ya kutoa maoni juu ya miswada hiyo kabla ya kuwa sheria.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks