Beki Sergio Ramos amesema kuwa timu ya Real Madrid imekuwa bora chini ya kocha Carlo Ancelotti kuliko ilivyokuwa kipindi cha kocha Jose Mourinho.
Ancelotti alichukua nafasi ya kocha Jose Mourinho kwenye msimu wa mwaka 2013 na kuisadia timu hiyo kunyakua ubingwa wa kombe la mabingwa ulaya.
Kwasasa kocha huyo amekalia kuti kavu kwenye klabu hiyo kutokana na kikosi chake kutokuwa na kiwango kizuri msimu huu.
Sergio anahojiwa kwenye kituo cha habari cha Cadena alisema Ancelotti atabaki kuwa mmojawapo wa makocha bora milele.
Mchezaji huyo aliongeza kuwa huwezi kumlinganisha kocha Ancelottina pamoja na Jose Mourinho na ninafikiri kwasasa timu yetu ni bora kuliko ilivyokuwa katika kipindi cha Mourinho ukitaka kujua kuwa Ancelotti ni bora angalia kupitia kwa mashabiki na kwenye vyombo.

0 comments:
Post a Comment