WHO yatangaza vita na makampuni ya sigara


Mkurugenzi wa WHO, Margaret Chan
Mkurugenzi wa WHO, Margaret Chan
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Margaret Chan ametoa wito siku ya Jumatano kuitaka dunia kuondoa tumbaku katika biashara na kusisitiza mafanikio ya kuachana na uvutaji katika mataifa mengi.
Akizungumza katika Mkutano wa Ulimwengu dhidi ya Tumbaku au Afya mjini Abu Dhabi, Chan alikaribisha mapendekelo yaliyotolewa na mataifa kadhaa, ikiongozwa na Australia, iliyoanzisha kutoa pakeji tupu za sigara.
Alitaka hatua hizo kufanywa na mataifa mengine.
Makampuni ya tumbaku “hutumia mbinu mbalimbali zikiwemo kuvipa fedha vyombo vya siasa, wanasiasa binafsi kufanya kazi kwa ajili yao… hawatoacha kufanya kuzorotesha jitihada za serikali kutaka kuokoa watu wao,” Chan aliwaambia waandishi wa habari.
Picha ikionyesha sigara ikimzika mvutaji sigara
Picha ikionyesha sigara ikimzika mvutaji sigara
“Yatakuwa mapambano makali… lakini hatupaswi kukata tama mpaka tuhakikishe biashara ya tumbaku inatokomea,” alisema.
Pamoja na kushuka kwa idadi ya wavutaji katika mataifa mengi, jitihada zaidi zinapaswa kufanyika kupambana na matumizi ya tumbaku ili kupunguza matumizi kwa asilimia 30 ifikapo 2025,” walisema washiriki.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks