Siku chache baada ya kuzinduliwa kwa treni mpya ya abiria ambayo inafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma,Watumiaji wa chombo hicho wamekosa ustaarabu baada ya kufanya uharibifu katika baadhi ya mabehewa.
Meneja wa treni hiyo Jonas Afumwisye, amesema baada ya kufika Kigoma, waliifanyia ukaguzi, ndipo wakagundua kuwepo kwa uharibifu katika baadhi ya vyumba vya daraja la pili na sehemu ya daraja la tatu la treni hiyo.
Hatua hiyo imewasikitisha viongozi wa Kampuni ya Reli (TRL), ambao wamekusudia kuongeza safari za treni hiyo kutoka mbili hadi tatu kwa wiki.

0 comments:
Post a Comment