![]() |
Vincent Kompany
|
1973: Roberto Carlos azaliwa
Jina lake halisi ni Roberto Carlos da Silva Rocha. Ni mchezaji wa soka kutoka nchini Brazil ambaye kwa sasa ni Kocha wa klabu ya Akhisar Belediyespor, ya nchini Uturuki.
Alizaliwa Garca katika jiji la Sao Paulo na kuanza kucheza kabumbu mwaka 1992. Alipachikwa jina la el hombre bala yaani mwanajeshi au mtu wa kazi. Alikuwa akicheza safu ya ulinzi ya kushoto, haijawahi kutokea katika timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Real Madrid mchapakazi kama huyo katika nafasi hiyo.
1984: David Obua azaliwa
David Obua ni mchezaji wa soka kutoka nchini Uganda ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Hearts of Middlelothian inayoshiriki ligi kuu ya Uskochi.
Hucheza nafasi ya winga ya kushoto. Alizaliwa jijini Kampala, Uganda. Amewahi kuzitumikia Kaizer Chiefs, kabla hajatua Hearts alifanya majaribio West Ham United ya England lakini akawahiwa na wakali hao wa Edinburgh.
1986: Vincent Kompany azaliwa
Vincent Jean Mpoy Kompany ni mchezaji kabumbu kutoka nchini Ubelgiji akiitumikia klabu ya Manchester City ya England katika nafasi ya kati ya ulinzi.
Alizaliwa Uccle, jijini Brussels. Alianza soka lake akiwa na umri wa miaka 17, katika klabu ya Anderlecht baadaye alitua Hamburg ya Ujerumani mwaka 2006.
0 comments:
Post a Comment