LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 11


1991: Alcantara azaliwa
Thiago Alcântara do Nascimento ni mchezaji wa kabumbu kutoka nchini Hispania. Kwa sasa anaitumikia klabu ya Bayern Munich. 

Hivi karibuni alitupia bao muhimu lililowavusha Bavarians dhidi ya Leverkusen katika Kombe la Ligi ya Ujerumani (DFB Pokal) licha ya kumchezea vibaya Stefan Kiessling.

 Alizaliwa  San Pietro Vernitico nchini Italia. Amefunga mabao 2 tu tangu atue Allianz arena mwaka 2013 akicheza mechi 17.

2005: Lucien afariki dunia
Lucien Laurent ni msakata kabumbu wa zamani kutoka nchini Ufaransa. Mkali huyu aliweka rekodi ya kuwa mfungaji wa kwanza wa bao katika Kombe la Dunia. Lucien alifunga bao hilo katika dakika ya 19 nchini Uruguay mwaka 1930.

Alizaliwa Desemba 10, 1907 katika kitongoji cha Saint-Maur-des-Fossés kusini magharibi mwa Jiji la Paris. Alifariki  akiwa na umri wa miaka 97  katika mji mkuu wa mkoa wa Franche-Comté, Besançon.

2014: Bill Henry afariki dunia
Akiwa na umri wa miaka 86, Bill Henry mkali wa mchezo wa Baseball kutoka nchini Marekani alifariki dunia mjini Round Rock katika jimbo la Texas kutokana na maradhi ya moyo yalikuwa yakimsumbua. 

Alicheza Ligi Kuu ya Baseball nchini humo (MLB) kuanzia 1952-1969 akiwa na Boston Red Sox, Chicago Cubs, Cincinnati Reds, San Francisco Giants, Pittsburgh Pirates, na Houston Astros katika nafasi ya kushoto ya uwanja
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks