Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ataikabili Eibar Jumamosi baada ya kuwa na kadi ya njano, na kufungiwa, imetenguliwa.
Ronaldo, ambaye amefunga magoli 37 katika mechi 27 za La Liga, alikabiliwa na adhabu ya mechi moja baada ya kutahadharishwa kujirusha dhidi ya Rayo Vallecano siku ya Jumatano.
Taarifa ya Real ilisema kamati ya mashindano ya shirikisho la soka la Hispania “limefuta kadi ya njano ya mwamuzi.”
Naye Gareth Bale atakosa kutokana na majeruhi wakati Real wakijaribu kupunguza pengo la alama nne la Barcelona kwenye msimamo wa ligi.
Ronaldo alipewa kadi ya njano ya tano kwa kujirusha kwenye eneo la penati wakati Real Madrid iliposhinda 2-0 dhidi ya Rayo Vallecano.
0 comments:
Post a Comment