Mkapa atoa ushauri kwa viongozi wa Afrika


Rais mstaafu Benjamin William Mkapa
Rais mstaafu Benjamin William Mkapa
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa amezitaka nchi za Kiafrika kuimarisha uongozi bora na kuachana na mikataba mibovu isiyojali ustawi wa wananchi kwa kuwa inaweza kuzipeleka nchi hizo kwenye vita.
Miongoni mwa mikataba ambayo  Mkapa amesema kuwa ni mibovu na isiyofaa, hivyo iepukwe ni mikataba ya Kiuchumi baina ya Mataifa ya Afrika, Caribbean na Pacific ili kuepusha vita, ambavyo kwa sasa vitakuwa ni vya kiuchumi.
Aidha Mkapa ametaka muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ufanyiwe marekebisho ili kuongeza nchi nyingine ambazo zinastahili kuingia kwa sasa.


Pia amesisitiza kuwa kwa hali ilivyo sasa ni sababu za kiuchumi ndizo zinazoleta vita, kutokana na uongozi mbaya, njaa na kiu ya baadhi ya nchi kutaka maliasili za mataifa mengine.
Share on Google Plus

About nellychazzy

I Run And Own Nellychazy.blogspot.com. Working With Web Editing, Blogs Template Fix And Editing (HTML). Monitoring click4hosting.net Deals with Web hosting. Also Base On Software And Hardware, Phones,Computer
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Blogger Tricks