Manny Pacquiao na Thomas Bradley 2014
|
1980: Marekani yagomea Olimpiki
MASHINDANO ya Olimpiki ya mwaka 1980 yalikuwa yakifanyika kwa mara ya kwanza katika Ulaya ya Mashariki.
Marekani iliongoza mgomo huo wa nchi 65 chini ya Rais Jimmy Carter wakipinga kufanyika huko kutokana na USSR kuwa vitani dhidi ya Afghanistan.
Licha ya mgomo huo lakini wanariadha wachache kutoka katika nchi zilizoitisha mgomo walihudhuria chini ya bendera ya olimpiki.
Kugoma kwa Marekani mwaka 1980 kuliamsha hasira ambapo Russia nayo iligoma katika Mashindano ya Olimpiki ya mwaka 1984 yaliyofanyika nchini Marekani.
2014:Pacquiao asheherekea kushinda WBO
BAADA ya Timothy Bradley kushinda ‘kimagumashi’ Juni 9, 2012 dhidi Manny Pacquiao walirudiana tena Aprili 12, 2014 katika ukumbi wa MGM Grand Arena na Mfilipino huyo aliuchukua tena mkanda wa WBO. Siku moja baada ya kuutwaa alisheherekea kuupata tena mkanda huo.
2014:Kipsang ashinda London Marathon
MBIO za London Marathon zilifanyika katika viunga vya jiji la London, England kukishuhudiwa mkenya Wilson Kipsang akinyakua taji la kilometa 42.2 akifukuza upepo kwa saa 2:04.29.
Kipsang wakati anatwaa taji hilo ilikuwa siku ya Jumapili katika mbio hizo za 34 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1981.
0 comments:
Post a Comment