Zaidi ya wasichana 400 wenye umri kati ya miaka 19-30 wametajwa kufika katika vituo vya afya katika kipindi cha mwezi July hadi Augosti mwaka huu kwa ajili ya utoaji mimba jambo linalosabisha ongezeko la tatizo la ugumba na vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini Tanzania.
Takwimu hizo zimezotolewa hii leo katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Afya ya Uzazi Dkt. Luzango Maembe, ambapo zinaonyesha asilimia kubwa ya wanawake hutoa mimba mitaani kwa kutumia njia za kienyeji pia wataalamu wasio na ujuzi hali inayopelekea wapate matatizo ya kudumu.
Takwimu hizo zimezotolewa hii leo katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Afya ya Uzazi Dkt. Luzango Maembe, ambapo zinaonyesha asilimia kubwa ya wanawake hutoa mimba mitaani kwa kutumia njia za kienyeji pia wataalamu wasio na ujuzi hali inayopelekea wapate matatizo ya kudumu.
Dkt. Maembe amesema kila siku wanapokea wagonjwa wawili wenye tatizo la kuharibika kwa mimba licha ya kuwepo wengine ambao huwa hawaripoti hospitalini na kuitaka jamii kuzingatia elimu ya afya ya uzazi pamoja na kuondokana na tabia ya kutumia njia zisizo salama.
“kati ya wagonjwa 200 wanaoletwa katika wodi ya wakinamama zaidi ya sitini au sabini wanakutwa na tatizo la mimba kuharibika au kutoa mimba kwa njia za kienyeji” alisema Maembe
Akizitaja baadhi ya njia zisizo salama zinazotumika kuwa ni pamoja na spoku za baiskeli utomvu wa mti wa muhogo, vyuma vyenye ncha kaali na vidonge, na kuwa utaratibu huo hufanyika bila kufuata maelekezo ya madaktari.
Aidha Dkt. Maembe amesema takribani kila siku wanapokewa wagonjwa wawili ambao wanamatatizo ya kuharibika kwa mimba na kuwa kati ya wasichana 25 kati yao watano wanatajwa kutoa mimba kwa njia rasmi na zisizo rasmi.
Katika zahanati na hospital kuwa za wilaya jijini Dar es salaam zinaonyesha asilimia kubwa ya wanawake hutoa mimba mitaani kwa kutumia njia za kienyeji pia wataalamu wasio na ujuzi.
Kulingana na utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha afya Muhimbili mwaka 2012 kuhusu utoaji wa mimba uliofanyika katika kata za wilaya ya Temeke ulionyesha asilimia 33 ya wasichana walipata mimba zisizotarajiwa . Kati yao asilimia 26 walizitoa, asilimia 87 zilitolewa kwa njia zisizo salama.
Wasichana zaidi ya 400 wenye umri kati ya miaka 19 na 25 waliohojiwa na kukiri kutoa mimba kwa msaada wa marafiki wa kiume, ndugu au wahudumu wa afya.
Kitaifa takwim zinaonyesha asilimia 18 ya mimba 2, 430,000 zilitolewa kiholela zilisababisha vifo.
Katika hospitali ya Amana na Temeke wanawake 444 walifikishwa kutokana na kesi za utoaji mimbavichochoroni tangu Januari hadi Juni mwaka huu.huku miongoni mwa wanaotoa mimba hizo ni wasichana wadogo na wanafunzi.
Uchunguzi unaonesha idadi kubwa ya wanaotoa mimba kiholela, hupata madhara mbalimbali ikiwamo kutoboka utumbo, kuchanika kwa kizazi, kuoza na wengine kuharibu figo.
Dkt. Chande Makaranga kwa uponde wake yeye analeza vitendo hivyo kuwa ni hatari kwa wanawake wanaotegemewa kuchangia kiasi kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa taifa kwani wakipatwa na madhara hayo ni vigumu kuchangia katika uchumi hata kujenga familia kwa kupata watoto.
0 comments:
Post a Comment