Javier Hernandez amedhihirisha kuwa aliondoka Manchester United kwenda Bayer Leverkusen kwa sababu alihitaji kuwa mwenye furaha tenaa.
Mshambuliaji wa Mexico, ambaye alikaa msimu mzima kwa mkopo Real Madrid, amesaini mkataba wa miaka mitatu baada klabu hizo kukubaliana uhamisho wa pauni milioni 12.
Hernandez alikuwa benchi katika mechi ya ambayo United ilifungwa 2-1 na Swansea siku ya Jumapili.
Hernandez alitambulishwa mbele ya waandishi wa habari siku ya Jumanne na alisema: “Nataka kwenye hisia za kuwa muhimu na mwenye furaha tena. Nataka kupata furaha.”
“Bayer wamefanya nijihisi nina umuhimu na kupendwa na kuja hapa haukuwa uamuzi mgumu kuufanya.’
“Wamefanya nihisi nahitajika,” aliongeza Chicharito, 27.
0 comments:
Post a Comment