Klabu ya Arsenal ya Uingereza ambayo kwa siku za hivi karibuni imeripotiwa kutafuta mshambuliaji wa kati, lakini ikawa inahusishwa kutaka kumsajili Karim Benzema kabla ya kocha wa Arsenal Arsene Wenger kukata tamaa ya kumpata nyota huyo, hivyo Wengeryupo Paris Ufaransa ili kupata mshambuliaji mbadala.
Picha nyingi zilizoenea mtandaoni siku ya Septemba 1, ni picha za kocha huyo akiwaParis Ufaransa na moja kati ya picha hizo, inaonyesha akiongea na mtu anayedhaniwa kuwa Edinson Cavani ambaye amekuwa akihusishwa kuwa katika mipango ya Arsene Wenger kwa siku kadhaa sasa.
Klabu ya Arsenal inahusishwa kutaka kuwasajili kiungo wa PSG Adrien Rabiot na mshambuliaji wa PSG kutokea Uruguay Edinson Cavani, ambaye usiku wa August 31 kuna picha ambazo zilipigwa kiwizi zikimuonyesha Arsene Wenger akiongea na mtu anayedahaniwa kuwa Cavani… Wenger yupo Ufaransa ili kukamilisha usajili wa wachezaji hao kwani zimesalia saa sio zaidi ya nne dirisha la usajili Uingereza lifungwe.
0 comments:
Post a Comment